Monday, 17 March 2008

Send off party-16 March 2008






Tarehe 16 March 2008, watanzania wenzetu wa Montreal, ambao tumeishi nao kwa takribani miezi 18 walitufanyia sherehe fupi ya kutuaga mimi, mke wangu na watoto wetu. Ama sina la kusema zaidi ya kumwomba Mola awazidishie watu hawa ambao walitufanya tujisikie tuko nyumbani. Katika hafla hiyo fupi, kwa ukarim wa hali ya juu, tulipewa Zawadi. Kila nikiiona zawadi niliyopewa, hupata picha ya jinsi nilivyoishi nawo. Mungu wabariki sana. Picha ya Juu kabisa nikifungua zawadi ambayo nilipewa , Picha ya kati muda mfupi kabla hafla haijaanza na Picha ya chini ni group photo ingawa kuna wachache wanakosekana.

Sunday, 27 January 2008

Wednesday, 19 September 2007

Kingunge unajaribu kusema nini

Asalam alaykum ndugu wasomaji wa ukurasa huu

Natumai nyote mu wazima wa afya na kila mmoja wetu amekuwa akimshukuru Mungu kwa yale yanayompata. Najua kuwa wale pia ambao wanadhani Mungu amewatupa, nao husema Mungu nimekosa nini. Nilijifunza kuwa hakuna jambo linalotokea pasina sababu. Cha kufanya ni kumshukuru Mungu.

Baada ya Utangulizi huo, sasa nirudi kwenye mada husika. Wengi wa watanzania , walioko ndani na nje ya nchi wanaelewa nini kinaendelea katika siasa za nchi yetu. Huku raisi akiwa nchini Marekani kwenye ziara ya kikazi, kuna mambo mengine mengi yanatokea nyumbani na sisi kama wachambuzi wa mambo ni jukumu letu kulizungumzia hili.

Baada ya Mheshimiwa Zitto Zubeir Kabwe kupigwa kadi nyekundu kugusa nyumba ya kutunga sheria hadi January mwakani, tumeshashuhudia mambo mengi yakitokea. Moja ni ziara ya viongozi wa umoja wa vyama vinne vya upinzani TLP, NCCR, CUF na CHADEMA wamefanya ziara kubwaaa mikoani kuweza kuamsha hisia za watanzania katika kutetea na kulinda rasilimali zetu. Kitu ambacho nakiunga mkonono kwa vile hata wafisadi wanafanya hivyo kwa vile hizo rasilimali zipo. Zikiisha watakosa pa kuchota. Hawa wanatakiwa kumshukuru mtu anayetaka zisimalizwe haraka, angalau vizazi vijavyo navyo vipate. Naam, kabla ya ziara ya mikoani, tulisikia kauli mbali mbali za wanasiasa wa chama tawala wakijaribu kufafanua mambo kadhaa, hasa yaliyomsibu Zitto. Mmoja wa wanasiasa hawa ni Mheshimiwa John Samwel Malecela. Sina kumbukumbu kuhusu mzee Kingunge, lakini kwenye sakata la muafaka mzee huyo ambaye nimeanza kumsikia tangu sijaanza shule ya msingi miaka zaidi ya 20 iliyopita alisema kitu. Alizungumza na mazungumzo yake yalileta kitim tim kwa CUF kutaka kujiondoa.

Nimelazimika kusema haya kwa vile nataka kujenga hoja ya kwanini sijaelewa kile mzee Kingunge alidhamiria kusema katika kauli zake za siku za karibuni.

Ni katika hili la Dr. Slaa, Zitto na wenzake kuwataja wafisadi kule kwenye viwanja mwembetogwa Temeke. Kingunge, anasema kuwa kama akina Dr. Slaa na wenzake wana ushahidi wa wanayoyasema wapeleke kwenye vyombo husika ili washughulikiwe. Halafu akaendelea kusema kuwa wapinzani pamoja na uchache wao wanataka kila wanaloleta bungeni likubaliwe. Huyu mzee pamoja na kuwa nimeanza kumsikia nikiwa na miaka 9, na sasa ni zaidi ya miaka 25 tangu wakati huo, anashindwa kutofautisha kati ya hoja yenye nguvu na nguvu ya hoja. Eti mpaka muwe wengi bungeni ndo mambo yenu ya kubaliwe. Kwangu mimi hili halingii kichwani kuwa ili kitu kishughulikiwe bungeni unahitaji wabunge wengi. Tumefikia kwenye kupitisha hoja kwa idadi ya wabunge bila kujua athari zake kwenye taifa na rasilimali zake.

Kwa Kingunge yeye, ushahidi ni ule tu unaopelekwa mahakamani. Kwanza nani atamfunga paka kengele. Kingunge amesahau kuwa Dr. Slaa aliwasilisha hoja yake ya BOT na Spika akataka aridhishwe kwanza na baadae akaifanyia mzengwe , kitu ambacho kilifanya aiondoe hoja yake. Ni ushadidi gani anautafuta mzee huyu. Kasahau kuwa Zitto aliwasilisha hoja yake na kuambiwa kuwa kadanganya akafungiwa. Huyu mzee kasahau kuwa TAKUKURU wanasema hawawezi kuchunguza baadhi ya vigogo eti kwa vile wanalindwa na sheria. Amesahau kuwa kuiba hakuna kinga. Sasa anataka wapeleke ushahidi gani, na kwa nani. Mengi yamesemwa, lakini hakuna hatua zezote zilizochukuliwa na serikali. Hii inaonyesha ni kiasi gani ufisadi umekuwa na kinga ya ajabu nchini mwetu.

Mwisho wa yote ni kushtaki serikali kwa wananchi wake, walioichagua ili wajue la kuwafanya, hawa ni waajiri wa serikali, lazima wajue mfanyakazi wao anafanya nini. Nguvu ya hoja pekee ndo itaifanya serikali iwe makini na maamuzi yake.

Kwa mantiki hizo hapo juu, mimi binafsi sijaelewa Kingunge alitaka kusema nini. Napata wakati mgumu kuunganisha sentensi zake ili zilete maana. Labda kuna msomaji kampata atatusaidia hapa hapa kijijini.

Maasalam